Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ali Yasin al-Amili, Rais wa “Mkutano wa Wanazuoni wa Sur na maeneo yake,” katika hotuba aliyoitoa katika msikiti wa madrasa mjini Sur, alisisitiza kuwa kujadili suala la kukabidhi silaha za muqawama, ilhali serikali haina uwezo wa kujibu hata moja ya hujuma za Kizayuni, ni kujitumbukiza katika kujiua – jambo ambalo hakuna mtu mwenye akili timamu anayelifanya.
Akaongeza kwa kusema: “Maadamu sababu za kuwepo silaha hizi bado zipo, hakuna nafasi yoyote ya kujadili suala la kuzirejesha, hasa kwa kuzingatia kuwa tunashuhudia mauaji ya kinyama ambayo yametuzunguka kutoka kila upande, na wimbi la mauaji ya kisirisiri linaendelea katika maeneo yote ya Lebanon, na mradi wa Kizayuni-Amerika umefikia kiwango cha kikatili kisichowahi kufikirika katika ugaidi.”
Maoni yako